Ujerumani yasema inaitazama hali Venezuela kwa makiniUjerumani yasema inaitazama hali Venezuela kwa makini

17 Desemba 2025

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, amesema Ujerumani inafuatilia kwa karibu amri ya Rais wa Marekani Donald Trump, ya kuzuwia meli za mafuta zilizowekewa vikwazo zinazoingia na kutoka Venezuela.

https://p.dw.com/p/55YdG

Berlin 2025 |Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Ujerumani imeonya kuhusu hatua zozote zinazohatarisha amani na usalama wa kikanda.

Msemaji huyo amesema nia ya Ujerumani ni kuzuwia hali kuwa mbaya zaidi.

Awali Venezuela ilituma malalamiko yake rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kile ilichokiita “wizi” wa Marekani iliyodai imeiteka meli yake ya mafuta kwenye Bahari ya Karibiani wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *