“Unapokuwa na maji kidogo, kazi kubwa ni kuhakikisha haya maji hayapotei hovyo. Tumepewa maelekezo cha kwanza tuhakikishe tunafanya kazi mivujo yote inayopatikana kwenye maeneo yetu kusudi hiki kidogo kinachopatikana kiweze kuwafikia watu kwenye maeneo yao.

“Tuna ratiba ya upatikanaji wa maji, na Waziri amejaribu kutoa msisitizo na mwanzoni tulikuwa tunaandaa ratiba na eneo ni kubwa. Inapokuwa eneo ni kubwa ina maana maji yanasambaa kwenye eneo kubwa.

Na unaweza kukuta mtu mwingine anaweza kupata maji mapema kwenye muda ule tulizozungumza. Na mtu mwingine anaweza akatapa muda mchache kutokana na jinsi eneo lilivyo”- Mhandisi Mkama Bwire, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam DAWASA.
#LiveonClouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *