Wakati Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa tuzo za World travel awards mwaka 2026. Tanzania imekuwa king’ara katika tuzo hizo zilizofanyika desemba mwaka huu kwenye falme za Bahrain. Ambapo Tanzania ilishinda tuzo 5, tuzo ya Kituo Bora cha Safari, Hifadhi Bora ya Taifa Duniani, Kituo Bora cha Mikutano na Mapumziko ya Kibiashara Barani Afrika, kisiwa binafsi bora kwa Mapumziko na Serengeti Balloon Safaris iliyopo Arusha ikichukua tuzo ya Best Balloon Ride Operator Worldwide yani Mwendeshaji Bora wa Safari za Puto za Angani Duniani 2025,

Tuzo hizo za World Travel Awards zilianzishwa mwaka 1993 na zinatambuliwa duniani kote katika sekta ya utalii. Tuzo ya Mwendeshaji Bora wa Safari za Puto za Angani ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020, na kuanzia hapo hadi 2024 ilikuwa ikinyakuliwa na kampuni ya Dubai, Balloon Adventures Dubai. Lakini kwa miaka miwili sasa 2024 na 2025 kampuni ya kitanzania Serengeti Balloon Safari imeweza kuibuka kidedea na kuzishinda kampuni zingine kubwa za Afrika na dunia.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Meneja wa Biashara wa Serengeti Baloon safari Pascal Kirigiti, katika hafla iliyofanyika Bahrain. Aidha, Tanzania itakuwa mwenyeji wa Tuzo za World Travel Awards mwaka 2026.

#CloudsDigitalUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *