Watu watano wamefariki dunia na wengine tisa wameruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana, Desemba 16, katika eneo la Karasha mkoani Songwe, kwenye barabara kuu inayounganisha Mbeya na Tunduma.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe imesema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Mitsubishi Canter linalomilikiwa na kampuni ya Security Group Afrika, tawi la Mbeya, lililokuwa linatokea Tunduma, na gari aina ya Toyota Coaster lililokuwa linatokea Mbeya.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi