
Taarifa ya chama cha PPRD imesema kukamatwa kwa Shadary na upekuzi wa usiku kwenye makao makuu ya chama kunatia wasiwasi.
Kulingana na familia yake, Shadary, aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018, alikamatwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani alipo.
Kukamatwa kwake kunatokea katika mazingira ya kisiasa yenye mvutano, takribani miezi mitatu baada ya kiongozi wa chama hicho na rais wa zamani Joseph Kabila kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya uhaini.