
Afrika Kusini imewafukuza Wakenya Saba walioajiriwa na Marekani kama sehemu ya mpango wake wa kuwapa makazi mapya Waafrikana, Wazungu walio wachache. Hili haliwezekani kuboresha uhusiano ambao tayari ulikuwa mgumu kati ya Pretoria na Washington.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Gazeti la Kenya la Daily Nation linapitia hali hii ngumu hasa: “Utawala wa Rais Donald Trump unalenga kuwapokea maelfu ya Waafrika Kusini Wazungu nchini Marekani chini ya mpango wa kuwapa makazi mapya uliozinduliwa mwaka huu, kwa kuzingatia madai ya mateso ya rangi.” Madai ambayo Afrika Kusini inakanusha kabisa.
Afrika Kusini imewafukuza Wakenya Saba walioajiriwa na Marekani kama sehemu ya mpango wake wa kuwapa makazi mapya Waafrikana, Wazungu walio wachache. Hili haliwezekani kuboresha uhusiano ambao tayari ulikuwa mgumu kati ya Pretoria na Washington. Gazeti la Kenya la Daily Nation linapitia hali hii ngumu hasa: “Utawala wa Rais Donald Trump unalenga kuwapokea maelfu ya Waafrika Kusini Wazungu nchini Marekani chini ya mpango wa kuwapa makazi mapya uliozinduliwa mwaka huu, kwa kuzingatia madai ya mateso ya rangi.” Madai ambayo Afrika Kusini inakanusha kabisa.
“Kwa msingi huu, utawala wa Trump umetekeleza mpango unaowapa kipaumbele baadhi ya Waafrikana ili kupata hadhi ya ukimbizi nchini Marekani, kama ilivyokuwa mwezi Mei 2025 wakati kundi la kwanza lilipopokelewa kwa usaidizi wa ujumuishaji wao,” inasema La Nouvelle Tribune.
Wakenya saba waliofukuzwa waliingia nchini humo kwa visa za watalii na walikuwa wameanza kufanya kazi kinyume cha sheria, licha ya maombi ya awali ya visa za kazi kukataliwa. Daily Nation inachambua: “Wakati wa muhula wake wa pili, Trump alitoa shutuma za uwongo mara kwa mara kuhusu jinsi Afrika Kusini ilivyowatendea wazungu wake wachache, akizitumia kupunguza misaada kwa nchi hiyo na kuitenga Afrika Kusini kwenye mikutano ya G20.”
Washington, kwa upande wake, ilijibu haraka kuhusu kufukuzwa kwa watu hao: “Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliishutumu Pretoria kwa kuzuia shughuli zake za kuwapa wakimbizi makazi mapya, ikiita hali hiyo kuwa haikubaliki. Kwa upande wake, serikali ya Afrika Kusini inadai kuanzisha hatua rasmi za kidiplomasia na Marekani na Kenya ili kutuliza mzozo huo,” inahitimisha La Nouvelle Tribune.
Nchini Kenya, watu 18 walionaswa katika vita nchini Ukraine wamerejeshwa
Watu 18 walionaswa katika vita nchini Ukraine wamerejeshwa nchini humo, linaripoti Gazeti la Kenya la Daily Nation. Gazeti hilo linaelezea kwamba watu hawa 18 walirejeshwa kutoka Urusi, “wengine wakiuguza majeraha makubwa.” Mapema wiki hii, pia iligundulika kwamba angalau Wakenya 82 waliajiriwa kwa nguvu kupigana pamoja na jeshi la Urusi katika vita nchini Ukraine.
“Wengi, bila mafunzo yoyote ya kijeshi, hawajawahi kushikilia silaha maishani mwao kabla ya kuajiriwa. Baada ya kozi ya siku tano katika kambi za mafunzo, walipelekwa kwenye mstari wa mbele,” Gazeti la lLe monde linaelezea.
Mmoja wa wajitolea waliodanganywa, akizungumza na Daily Nation, anasimulia kwamba “mashirika kadhaa ya kuajiri yanadaiwa kuwapotosha waajiri hao wapya, yakiwaahidi kazi zenye faida kubwa katika usindikaji wa nyama, ufungashaji, na usafi,” huku yaakidai kufidia gharama za usafiri, uchunguzi wa kimatibabu, na malazi.
Na “Kenya sio nchi pekee ya Kiafrika inayoajiri,” linaelezea azeti la Le Monde Afrique. “Mamlaka ya Ukraine inakadiria kwamba zaidi ya wanajeshi 1,400 kutoka Afrika, kutoka nchini 36, wanapigana pamoja na jeshi la Urusi. Wengi wao kwenye uwanja wa vita chini ya shinikizo.”
Zaidi ya hayo, Kusini mwa Jangwa la Sahara “inaunda kundi kubwa na linalofikika kwa urahisi la waajiriwa kutokana na viwango vya juu vya umaskini katika nchi nyingi za eneo hilo” na “hamu kubwa ya kuhama,” kulingana na utafiti uliochapishwa leo Alhamisi hii na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya Ufaransa (Ifri).