Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 18 Desemba 2025 limekutana na uongozi wa Shirikisho la Michezo kwa Watu Wenye Ulemavu (Paralympic Tanzania) katika kikao cha pamoja kilicholenga kujadili maandalizi na uratibu wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo.
Katika kikao hicho, pande zote zimejadili kwa kina taratibu za uchaguzi unaolenga kupata viongozi wapya, kufuatia muda wa uongozi wa viongozi wa sasa kuelekea kuisha kwa mujibu wa Katiba ya shirikisho. Baada ya majadiliano, kikao hicho kimekubaliana kuwa uchaguzi mkuu wa Paralimpiki Tanzania utafanyika tarehe 26 Januari 2026, jijini Dar es Salaam.
BMT imeendelea kusisitiza umuhimu wa utawala bora katika kuimarisha maendeleo ya michezo kwa watu wenye ulemavu nchini.
#StarTvUpdate