Vifaa vya kijeshi vitakavyonunuliwa ni pamoja na nguo na vifaa vya kujilinda kwa ajili ya wanajeshi vyenye thamani ya yuro bilioni 21 na magari 200 ya kivita ya Puma yenye thamani ya yuro bilioni 4.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Berlin, Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius alisema uamuzi wa kuidhinisha matumizi hayo unaweka serikali na bunge katika mstari wa kutimiza ahadi za ulinzi.

Kamati hiyo ya bajeti bungeni ambayo husimamia manunuzi yote makubwa ya silaha, ina mamlaka ya kupitisha bajeti hiyo bila ya idhini ya bunge zima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *