Christian Bella apewa Uraia wa TanzaniaChristian Bella apewa Uraia wa Tanzania

MSANII maarufu wa muziki wa dansi wa Bongo, Christian Bella, amepewa uraia wa Tanzania baada ya kuishi na kufanya shughuli zake za muziki nchini kwa takribani miaka 20. Uamuzi wa kumpa uraia msanii huyo, anayefahamika kwa jina la kisanii “King of the Best Melodies”, umetangazwa leo Alhamisi, Desemba 18, 2025.

Akizungumza katika maahdimisho ya Siku ya Wahamiaji  Duniani,Waziri Simbachawene amesema Tanzania ina idadi kubwa ya wahamiaji wanaoishi na kufanya kazi kwa kufuata sheria, huku baadhi yao wakipewa uraia kutokana na mchango wao katika maendeleo ya taifa ikiwemo sekta ya sanaa na utamaduni.

Katika safari yake ya muziki nchini, Christian Bella aliwahi kujiunga na bendi ya Akudo Impact na kutoa wimbo unaojulikana kama  “Walimwengu Si Binadamu” uliomfungulia milango katika tasnia ya muziki wa Bongo. Msanii huyo alianza safari yake ya muziki akiwa kijana mwenye vipaji vingi, akishirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo Fally Ipupa, ambaye baadaye alijiunga na Koffi Olomide.

Akiwa na umri wa miaka 16, Bella alijiunga na bendi ya Koffi Olomide, lakini hakupata nafasi ya kutumbuiza jukwaani, hali iliyomfanya kurejea na kuendelea na Akudo Impact. Kabla ya kupewa uraia wa Tanzania, Christian Bella alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). SOMA: Christian Bella aachia albamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *