DAKTARI mmoja wa Ufaransa, Frédéric Péchier (53), amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwadunga sindano za sumu wagonjwa 30 kwa makusudi, ambapo wagonjwa 12 walifariki dunia.

Péchier alibainika kuwawekea wagonjwa wake kemikali hatari zikiwemo potassium chloride na adrenaline. Hii itakuwa kesi ya kwanza nchini Ufaransa ya ukiukwaji wa maadili ya kitabibu ambayo haijawahi kutokea nchini humo. Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa wiki iliyopita  katika mji wa Besançon, mashariki mwa Ufaransa, baada ya kesi iliyodumu kwa miezi minne.

Waendesha mashtaka walimuelezea Péchier kama “daktari muuaji,” wakisema, “Umedhalilisha taaluma nzima ya udaktari. Umeigeuza hospitali hii kuwa kaburi.” SOMA: Kaka na dada wafungwa jela kwa kuoana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *