#HABARI: Baadhi ya wafanyabiashara wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamesema uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kahama uliofanywa na Serikali, umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa fursa za kibiashara katika eneo hilo.

‎Wamesema kuongezeka kwa safari za ndege kupitia mashirika mbalimbali ya ndani ya nchi kumechochea ukuaji wa shughuli za biashara, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, pamoja na kuongeza mvuto wa uwekezaji katika Manispaa ya Kahama.

‎Wakizungumza na ITV katika Uwanja wa Ndege wa Kahama, wafanyabiashara hao wameeleza kuwa maboresho hayo yamepunguza muda wa usafiri, gharama za uendeshaji wa biashara na kuongeza kasi ya shughuli za kiuchumi.

‎Kwa upande wao, wadau wa sekta ya usafirishaji wa anga nchini wamesema kuongezeka kwa safari za ndege, hususan katika Uwanja wa Ndege wa Kahama, kumeongeza tija, kuimarisha huduma za usafiri wa anga na kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa Shinyanga na mikoa jirani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *