HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe mkoani Njombe imetoa tamko la kuunga mkono ushindi wa kishindo uliopatikana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Ambapo imewasisitiza Watanzania hawana budi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi hao, kwa kuwa Katiba ya nchi bado inaweka misingi ya kusikiliza maoni ya wananchi kupitia vikao vya kikanuni, kikatiba pamoja na mifumo mingine ya mashauriano ya kitaifa.