
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kulaani vitisho vya Marekani kwamba itaiwekea vikwazo vya baharini Venezuela na kuitaka hatua hiyo kuwa uharamia unaofadhiliwa na serikali.
Taarifa hiyo imelaani vitisho vya Marekani vya kuzuia usafirishaji halali wa mafuta ya Venezuela. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imevitaja vitisho vya Marekani kuwa dhihirisho wazi la sera iliyojikita katika “uonevu wa kimfumo na utumiaji mabau,” ambayo inajumuisha ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kanuni za uhuru wa kusafiri na biashara ya kimataifa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema: Jaribio lolote la Marekani la kukamata, kuzuia au kukwamisha usafiri huru wa meli za kibiashara zinazosafiri kwenda au kutoka Venezuela ni kitendo cha moja kwa moja cha “uharamia wa serikali na ujambazi wa kutumia silaha baharini.”
Taarifa hiyo imefafanua zaidi kwamba Marekani haiwezi kutumia sheria zake za ndani au vikwazo vya upande mmoja, kinyume cha sheria kuhalalisha vitendo hivyo vya uhalifu.