Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), imeibuka mshindi wa Tuzo ya Uwezesahaji Vijana na Ukuzaji Ujuzi (Youth Emporment and Skills Development) katika Tuzo za Ubunifu wa Sekta ya Umma mwaka 2025.

Tuzo hizo zimeltolewa na Bodi ya Tuzo za Ubunifu katika Sekta ya Umma katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.

Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua jitihada za ubunifu zinazofanywa na VETA katika kuwawezesha vijana na kukuza ujuzi, ikiwa nipamoja na kutoa ujuzi huo kupitia mifumo ya kidigitali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamis Suleiman Mwalimu, amesema tuzo hizo ni chachu ya kuimarisha ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya umma na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mkurugenzi wa Rasilimali wa Watu, Enihart Mahundi amesema VETA inawashuku waandaaji wa tuzo hizo kwa kutambua mchango wao katika kuwezesha vijana na kukuza ujuzi hapa nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo za Ubunifu katika Sekta ya Umma, Steven Mkomwa, amesema tuzo hizo zinafanyika kwa mara ya kwanza kwa lengo la kuhamasisha ubunifu, uwajibikaji na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *