#MICHEZO: Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania (Spata) Mussa Kisoky amejitokeza kwa mara ya pili kupinga adhabu mpya ya kuwafungia wachezaji Mechi 5 na kuwalaumu viongozi wa klabu kutokuwa makini wakati wa kupitia kanuni mpya kwani adhabu hiyo inaathiri maisha ya kisoka ya mchezaji kutokana na uwingi wa michezo atakayokosa!
Sasa wamefungiwa Mechi 5 Jonathan Sowah, Allasane Kante na Khalid Aucho lakini Mwenyekiti huyo alijitokeza mara ya kwanza kupinga wakati Ibrahim Bacca amefungiwa mechi 5 na kuitaka mamlaka ya soka Tanzania TFF kushirikisha Chama chao wachezaji Spata wanapoleta kanuni zinazohusu wachezaji.
@hoseamchopa