
Polisi nchini Uhispania Jumatano waliwafurusha mamia ya wahamiaji haramu waliokuwa wakiishi katika jengo la shule lililotelekezwa katika mji wa Badalona unaopakana na mji wa Barcelona kaskazini-mashariki mwa Uhispania.
Aghalabu ya wahamiaji hao haramu mapema jana asubuhi waliondoka katika jengo la shule hiyo iliyotelelezwa kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.
Polisi ya Uhispania imewafurusha wahamiaji hao haramu baada ya mamlaka husika za nchi hiyo kuamuru kuwa jengo hilo la shule halikuwa salama.
Younous Drame raia wa Senegal ambaye ni miongoni kwa wahamiaj haramu waliolazimishwa kuondoka katika jengo la shule katika mji wa Badalona huko Uhispania amesema kuwa walitumai kuwa wangeruhusiwa kubaki hapo angalau baada ya Sikukuu ya Krismasi au baada ya kumalizika msimu wa baridi kali.
“Inavunja moyo sana kuwafukuza watu 400 katika msimu huu wa baridi kali. Mtu wa aina hii lazima atakuwa na roho ngumu hadi kufanya hivi”, alisikika akisema raia huyo wa Senegal.
Wahamiaji wengi wasio na vibali, kutoka Senegal na Gambia walihamia katika jengo tupu la shule lililokuwa limetelekezwa tangu mwaka 2023.