Serikali imewataka maafisa maendeleo ya vijana nchini kutekeleza hatua za kimkakati zilizowekwa kwa lengo la kuimarisha mifumo ya sera, sheria na utendaji kuhusu maendeleo ya vijana ambayo nids chanson cha kuundwa kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Akizungumza na katika ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema kuwa lengo la uwepo wa wizara na maafisa hao ni kuboresha na kuimarisha ustawi wa vijana na maendeleo yao nchini.

“Ni lazima kuzingatia falsafa tatu (3) za wizara ambazo ni kasi ya kusikiliza na kufanyia kazi mawazo na ushauri wa vijana, kuwafikia vijana walipo na kuwasikiliza sambamba na kutumia teknolojia katika kushughulikia masuala yanayowahusu ili kuendana na kasi yao” Ameongeza Nanauka

Waziri Nanauka pia ameweka msisitizo kwa maafisa hao kukusanya na kutumia takwimu sahihi za vijana waliopo katika maeneo yao na waweze kutambua changamoto zinazowakabili vijana na kutafuta ufumbuzi.

“Pia ni lazima kuwaunganisha vijana na programu na fursa zote za kitaifa zinazohusu ujuzi, ajira na uwezeshaji wa kiuchumi.” Amesisitiza Nanauka

Kikao hicho cha Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri kinalenga kuwajengea uelewa wa kina wa majukumu ya kuendeleza vijana.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *