Nchini Sudan, miezi miwili baada ya kutekwa kwa mji wa El-Fasher, huko Darfur, na vikosi vya kijeshi vya Jenerali Hemetti, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale wanasema wamegundua maeneo 150 yanayofanana na makaburi ya halaiki kote jijini. Maeneo haya yalitambuliwa kupitia uchambuzi wa picha za setilaiti zilizopigwa kila baada ya saa 24 kuanzia mwisho wa mwezi wa Oktoba, wakati jiji lilianguka mikononi mwa waas wa RSF, hadi mwisho wa mwezi Novemba. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyochapishwa mnamo Desemba 16, Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu ya Yale inakadiria kwamba wanamgambo wa RSF waliharibu na kuficha ushahidi wa mauaji makubwa. Idadi ya vifo inakadiriwa kuwa makumi ya maelfu.

Maeneo mia moja na hamsini yanayofanana na makaburi ya halaiki yametambuliwa ndani na karibu na jiji la El-Fasher, katika Jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan. Theluthi moja ya maeneo haya yapo Daraja Oula, kitongoji cha mwisho ambapo raia wengi walikimbilia kabla tu ya jiji kuanguka mikononi mwa wanamgambo wa RSF.

Makaburi haya ya halaiki, ambayo yalionekana katika maeneo mbalimbali ndani ya mji huu wa El-Fasher kwa siku kadhaa, yanaonyesha, kulingana na watafiti, kwamba wanajeshi walitembea katika eneo hilo, wakiwaua raia waliokuwa wamejificha katika nyumba zao. Maeneo themanini na matatu pia yalitambuliwa nje ya jiji, kando ya barabara. Hii, kulingana na watafiti, ni ushahidi kwamba raia waliuawa wakati wakijaribu kukimbia.

Ripoti pia inaonyesha athari za moto katika maeneo ishirini hivi, ikionyesha kwamba miili ilichomwa. Katika maeneo mengine manane, kiasi kikubwa cha ardhi kimevurugwa. Uchambuzi wa picha za setilaiti kwa mwezi mmoja pia unaonyesha kwamba baadhi ya makaburi ya halaiki yametoweka. Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu ya Yale inabaini RSF waliharibu na kuficha ushahidi wa mauaji makubwa, anaelezea mmoja wa watafiti, Olivia Mooney, amemuelezea mwandishi wa habari wa RFI, Alexandra Brangeon.

Maeneo haya, ambayo tumeyatambua kama makaburi ya halaiki, yanapatikana hasa katika maeneo mawili.

Ingawa hawawezi kutoa idadi kamili ya vifo, watafiti wa Yale wanahitimisha kwamba kulikuwa na mauaji ya halaiki, ambayo huenda yalihusisha makumi ya maelfu ya raia. Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kibinadamu huomba mara kwa mara ufikiaji wa El-Fasher, ambapo mawasiliano bado hayajakamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *