Zaidi ya raia 1,000 waliuawa mwezi Aprili katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Zamzam huko Darfur Kaskazini, Sudan, wakati wa shambulio la wanamgambo wa RSF, ambao wamekuwa wakikabiliana na jeshi tangu mwezi Aprili 2023, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ilmetangaza leo Alhamisi Desemba 18, 2025.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu imeelezea “mauaji ya halaiki, ubakaji na ukatili mwingine wa kingono, vitendo vya mateso na utekaji nyara” vilivyofanywa wakati wa shambulio hilo, ambalo lilifanyika kuanzia Aprili 11 hadi 13 na kutekelezwa na Vikosi vya Msaad wa Haraka (RSF). Kulingana na Umoja wa Mataifa, “angalau raia 1,013 waliuawa.”

Hivi karibuni Mkuu wa OHCHR alitaka mapigano yakome mara moja Sudan akilaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumza mjini Geneva Uswisi Türk  amesema “Nina wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa mapigano kati ya Jeshi la Sudan, Vikosi vya Msaafa wa Haraka, na Kundi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini SPLM-N, katika eneo la Kordofan,”

Türk, meihimiza pande zote katika mzozo huo wa Sudan na Mataifa yenye ushawishi kuchukua hatua thabiti mara moja.

Tangu 4 Desemba, raia takriban 104 wamepoteza maisha katika mashambulizi kadhaa ya Ndege zisizo na rubani au droni katika eneo hilo.

Katika shambulio moja la kusikitisha lililolenga shule ya chekechea na hospitali katika eneo la Kalogi, Kordofan Kusini, mkuu huyo wa Ofisi ya Haki za Binadamu amesema raia 89 wakiwemo wanawake wanane na watoto 43 waliuawa.

Türk pia amekosoa vikali mauaji ya walinda amani sita wa wa Umoja wa Mataifa katika shambulio la droni kwenye kambi ya Umoja wa mataifa huko Kadugli tarehe 13 Desemba.

Alionya kuwa “Kuongoza na kufanya shambulio dhidi ya wafanyakazi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kunaweza kuwa ni uhalifu wa kivita”.

Hali ya ghasia iliendelea tarehe 14 Desemba, wakati shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye hospitali huko Dilling liliripotiwa kuua angalau watu sita na kujeruhi wengine 12, wakiwemo wafanyakazi wa afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *