
TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 imefanya mahojiano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, kujadili matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi hicho.
Katika mahojiano hayo yaliyofanyika leo Desemba 18 katika Ofisi za muda za Tume hiyo, Chalamila ameridhishwa na zoezi hilo la ukusanyaji wa taarifa za matukio ya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi Oktoba 29 .

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na chanzo cha matukio ya uvunjifu wa amani, athari zake kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na uharibifu wa mali na miundombinu. SOMA: Tuipe ushirikiano Tume ya Uchunguzi
Tume imeeleza kuwa itaendelea kufanya mahojiano na waathirika wa matukio hayo kwa lengo la kubaini kwa kina chanzo cha vurugu hizo na kupendekeza hatua stahiki za kitaifa ili kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena.