Umoja wa mataifa na mashirika hayo wamesema kwenye taarifa yao ya pamoja kwamba shughuli hizo huenda zikafungwa ikiwa Israel haitaondoa vizuizi ambavyo ni pamoja na mchakato mgumu wa usajili.

Taarifa hiyo imesema hatua ya kufutwa kwa usajili wa mashirika ya misaada ya kimataifa huko Gaza itakuwa na athari kubwa katika upatikanaji wa huduma muhimu na za msingi.

Mashirika mengi ya misaada ya kimataifa huenda yakafutiwa usajili hadi kufikia Disemba 31, hii ikimaanisha kwamba yanapaswa kufunga shughuli zao ndani ya siku 60.

Mashirika hayo yanasaidia huduma za tiba, makazi ya dharura, huduma za maji na usafi wa mazingira na vituo vya lishe kwa watoto wenye utapiamlo mkali, miongoni mwa nyinginezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *