
Hayo yameelezwa na vyanzo vya kiusalama katika eneo hilo, baada ya kundi hilo la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda kutangaza kuwa limeanza kujiondoa katika mji huo na kuahidi kuwa zoezi hilo linatarajiwa kukamilika leo Alhamisi.
Tangu kutolewa kwa tangazo hilo, serikali ya Kongo na hata baadhi ya wakazi wa Uvira wameelezea mashaka yao, wakisema huenda hatua hiyo ni mbinu ya M23 ya kuipotosha jumuiya ya kimataifa, huku wakitoa wito wa tahadhari.