
Bertrand Bisimwa, kiongozi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda ameliambia shirika la habari la AP kwa njia ya simu kwamba hatua hiyo inakamilika asubuhi ya leo.
Hata hivyo, msemaji wa Gavana wa Kivu Kusini hakupatikana kuthibitisha taarifa hizo.
Waasi wa M23 walichukua udhibiti wa mji huo wiki iliyopita kufuatia mashambulizi iliyoyaanzisha mapema mwezi huu licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani na kusainiwa na marais wa Kongo na Rwanda.