Waasi wa kundi la M23 hawajaondoka katika mji wa Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya mapema wiki hii kutangaza kuwa wataondoka katika mji huo.

Willy Ngoma Msemaji wa waasi wa M23 jana aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba wako tayari kuondoka Uvira lakini masharti yao lazima yapitiwe upya. 

Ngoma ameongeza kuwa: Wakazi wa mji wa Uvira walihitaji kulindwa na kwamba mji huo ulihitaji kuwa chini ya udhibiti wa kikosi kisichoegemea upande wowote. 

Jumatatu wiki hii waasi wa M23 walisema kuwa wataondoka huko Uvira ili kusaidia juhudi za Qatar na wasuluhishi wengine ili kurejesha amani katika vita vya muda mrefu kati yao na vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Kundi la M23 liliingia katika mji wa Uvira karibu na mpaka wa Burundi mapema mwezi huu yaani chini ya wiki moja baada ya Marais wa Kongo na Rwanda kukutana Washington na Rais Donald Trump wa Marekani ili kuthibitisha utayarifu wao kwa mikataba ya amani ya Washington. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *