
TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imeendelea kwa siku ya nne kusikiliza ushahidi wa majeruhi, ndugu wa wafiwa na waliopoteza mali zao.
Mahojiano hayo yamefanyika Katika Ukumbi wa Karimjee mkoani Dar es Salaam ikiwa ni kikao cha wazi na wananchi. Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande na jopo lake walihoji juu ya mazingira, maeneo na muda wa matukio ya baadhi ya majeruhi walivyojeruhiwa.

Baadhi ya waathirika wa ghasia hizo wameiomba serikali kuhakikisha Jambo hilo halijirudii tena kwa kuwawezesha vijana mikopo au ajira ili wakose muda wa kufanya matukio kama ya Oktoba 29. SOMA: Tume ya Uchunguzi ina ‘kibarua kizito’ lakini muhimu