
Takriban watu 12 wameuawa na wengine watatu kutekwa nyara baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo la uchimbaji madini katika kijiji cha Atoso katika jimbo la Plateau nchini Nigeria.
Dalyop Solomon Mwantiri kiongozi wa kundi la kiraia anayeongeza Jumuiya ya Vijana ya Berom Moulders-Association (BYM) ameeleza kuwa wavamizi ambao wametajwa na wenyeji kuwa ni wanamgambo wa kabilal la Fulani walifanya hujuma hiyo Jumanne jioni na kusababisha watu wengine watano kulazwa hospitali kutokana na majeraha ya risasi.
Msemaji wa Polis, Alfred Alabo amethibitisha kuwa uchunguzi umeanza kuhusu shambulio hilo latika eneo la uchimbaji madini huko Atoso katika jimbo la Plateau.
Shambulio hili linadhihirisha ukosefu wa usalama unaoendelea katika jimbo la Plateau nchini Nigeria; eneo lenye hali tete kaskazini kati la nchi hiyo ambapo mizozo ya kikabila na kidini kwa muda mrefu sasa imekuwa ikichochea mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji.
Hali ya ukosefu wa usalama inaendelea kulitatiza jimbo la Plateau nchini Nigeria licha ya serikali kuaahidi mara kwa mara kurejesha amani jimboni humo.