Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha katika kipindi hiki cha mpito, ratiba ya mgao wa maji inakuwa wazi, inayotekelezeka, shirikishi na inayowafikia wananchi wote ili kila mmoja apate maji yaliyopo kwa wakati.

Waziri Aweso amesisitiza kuwa uwazi katika ratiba hiyo utasaidia kupunguza malalamiko kwa wananchi na kuwezesha kufanya matumizi bora ya maji wanayoyapata.

#AzaTVUpdates
✍Nifa Omary
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *