Rais Zelensky amesema hayo kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya unaofanyika Alhamisi mjini Brussels.

Zelensky amesema matokeo ya mikutano kama hiyo yanatakiwa kuifanya Urusi kuona hakuna maana yoyote ya kuendeleza vita hadi mwaka ujao kwa kuwa Ukraine itakuwa na uungwaji mkono.

Ametoa wito huo huku Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz akiurai Umoja wa Ulaya kutumia mali za Urusi zilizozuiliwa kuisaidia Ukraine, “kuongeza shinikizo kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin” na “kutuma ishara ya wazi kwa Urusi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *