NAIROBI – Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, katika ripoti yake ya hivi punde limesema polisi nchini Tanzania walitumia nguvu kupita kiasi kudhibiti waandamanaji kipindi cha uchaguzi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Amnesty inasema vitendo vya polisi wa Tanzania vinaonesha hali ya kutisha ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwemo haki ya kuishi na kukusanyika, kwani idadi kubwa ya waandamanaji waliuawa wakati wa maandamano hayo.

Mmoja wa wahudumu wa afya aliyezungumza na Amnesty amekiri kuiona miili ya watu waliouawa kwa kupigwa risasi ikiliwa na mwewe katika jiji la Dar es Salaam.

Katika ripoti yake, Amnesty imesema polisi walitumia risasi kuwalenga waandamanaji na raia wengine ambao hawakuwa wakiandamana, na pia walirusha vitoa machozi katika makaazi ya raia. Amnesty sasa inaitaka serikali kuzipa familia miili ya wapendwa wao ili kufanyiwa maziko.

Serikali ya Tanzania imeuunda tume kuchunguza kilichojiri kipindi cha uchaguzi,ila  Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International, amesema kuna haja ya tume hiyo kuhakikisha haki inatendeka na kwamba haifai kuegemea upande wowote, licha ya mashirika ya kiraia nchini Tanzania kuonesha kuwa hayana imani na tume hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *