Balozi wa Palestina anayeiwakilisha nchi yake Tanzania Salim Siam amehimiza wanahabari wa Tanzania kuonesha mshikamano na Palestina, ili kupaza sauti ya pamoja kukemea mateso wanayofanyiwa raia wa Palestina na majeshi ya IsraeL.

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa DAR-PC Balozi Siam amesema Wapalestina wanahitaji nguvu ya pamoja katika kukemea maovu hasa mauaji yanayoendelea katika eneo la Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ambayo yamegharimu maisha ya watu wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto.

Amesema tangu kuanza kwa mashambulizi hayo Oktoba 2023, tayari Wapalestina 70,663 wameuwa kufikia wiki hii ya Desemba 15 mwaka huu, wakiwemo wanahabari 256 na kuharibu kabisa majengo, Barabara, vyanzo vya maji, vyanzo vya nishati, majengo ya hospitali, shule na vyuo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Wanahabari wa Dar es Salaam (DAR-PC), Andrew Msechu amesema wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu hali ilivyo Palestina na kwamba wanaendelea kuunga mkono msimamo wa Serikali katika kutambua na kuunga mkono upatikanaji wa Dola huru ya Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *