#HABARI: Jeshi la Polisi Nchini kupitia kikosi cha Usalama barabarani, limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria, kwa ajili ya kudhibiti ajali kutokana na ongezeko kubwa la abiria kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Joseph Mwakabonga, wakati akizungumza na madereva katika Stendi kuu ya mabasi Mkoani Arusha, amesema kuelekea mwisho wa mwaka kunajitokeza ajali kwa sababu madereva wengi wanakuwa na mihemko ya kutaka kusafirisha abiria wengi kwa muda mfupi.

ACP Mwakabonga amebainisha kuwa wanaendelea na operesheni hiyo nchi nzima ili kutoa elimu kwa madereva na abiria pamoja na kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto ili kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kama siyo kuisha kabisa.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *