#HABARI: Maboresho makubwa ya miundombinu yaliyotekelezwa na Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia Mradi wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP) yanaendelea kuzaa matunda, baada ya bandari hiyo kupokea meli kubwa na ndefu zaidi ya makasha kuwahi kutia nanga, yenye urefu wa mita 304.40.
Meli hiyo ya makasha, inayofahamika kwa jina la MSC STELLA, ina urefu unaolingana na viwanja vitatu vya mpira wa miguu vilivyopangwa mfululizo, tukio linalothibitisha hatua kubwa iliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam katika kuongeza uwezo wake wa kuhudumia meli kubwa kwa viwango vya kimataifa.
MSC STELLA imewasili kutoka Bandari ya Jebel Ali, Dubai, moja ya bandari kubwa duniani. Ujio wake unaipa Bandari ya Dar es Salaam heshima kubwa, unaongeza kujiamini kiutendaji na kiusalama, na kuendelea kuipambanua bandari hiyo katika ramani ya usafirishaji wa Kimataifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania