#HABARI: Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Hala, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Gabriel Noel (45), amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa kitu kizito na rafiki yake, Adam Keto, katika tukio linalodaiwa kusababishwa na ugomvi wa kadi ya kumbukumbu (memory card) ya simu.
Tukio hilo limetokea Desemba 17, 2025, katika mazingira ambayo chanzo chake kinaelezwa kuwa ni kugombania kadi ya kumbukumbu ya simu, kati ya marehemu na mtuhumiwa.
Baada ya kutekeleza tukio hilo, mtuhumiwa Adam Keto alikimbilia msituni, na hadi sasa hajafanikiwa kukamatwa, huku juhudi za kumtafuta zikiendelea kwa ushirikiano wa wananchi pamoja na viongozi wa kijiji hicho.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Hala kati Emanuel Hando amesema mtuhumiwa anadaiwa kuwa na historia ya vitendo vya uhalifu, ikiwemo kuwashambulia watu na kutoweka baada ya kutekeleza matukio hayo madai ambayo yapo chini ya uchunguzi wa vyombo vya usalama.
Hadi sasa, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, huku wananchi wakitakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili mtuhumiwa aweze kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.