#HABARI: Ng’ombe 22 wa mfugaji Alex Idege, mkazi wa Kijiji cha Kasingili, Kata ya Ilola wilayani Shinyanga, wamekutwa wamekufa zizini baada ya kurejea kutoka malishoni, katika tukio linalodaiwa kuwa na mazingira ya kutatanisha.
Mmiliki wa mifugo hiyo amesema saa 10 Alfajiri alisikia mifugo wakilia, akatoka nje kisha akamulika zizi akaona mifugo ipo na kurudi kulala, lakini saa 11 alikuja kijana kwa ajili ya kufunga ng’ombe kwa ajili ya kwenda kulima, ndipo akaona mifugo ikiwa imekufa na kumpatia taarifa.
Anasema baada ya kupewa taarifa hiyo alikimbia tena zizini ndipo akaona ng’ombe sita wakiwa wamekufa na wengine kuzidiwa, lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda waliendelea kufa hadi wakafika 22 na kubakiza ndama watatu ambao wenyewe hawakuenda malishoni.
“Mifugo yangu hua inakwenda kulisha eneo moja tu, lakini majibu ambayo nimepewa na mtaalamu wa mifugo anasema eti wamekula majani yenye sumu, majibu ambayo sijaridhishwa nayo kabisa, sasa hivi nimebakiza ndama watatu, ngombe wote 22 wamekufa,”amesema Idege.
Naye diwani wa Kata ya Ilola Kisena Fred, amesema amesikitishwa juu ya tukio hilo, na kuomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini vifo vya mifugo hiyo, na kama ni ugonjwa ni vyema hatua za haraka zichukuliwa kuudhibiti na kutoathiri mifugo ya wananchi wengine.
Kwa upande wake Ofisa Mifugo Kata ya Ilola Daniel Jilala, alisema tayari wameshachukua sampuli za mifugo hiyo, na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha vifo vya mifugo hiyo, lakini uchunguzi wa awali inaonyesha wamekula majani yenye sumu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.