#HABARI: Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Uratibu Mpango wa Uzalishaji Umeme wa Nyuklia Nchini (NEPIO) wametakiwa kuhakikisha wanaanza maandalizi mapema ya namna mpango huo utakavyotekelezwa Nchini huku akiwasisitizwa kuhakikisha wanazingatia matumizi ya rasilimali zinazopatikana nchini Tanzania katika utekelezaji wa mpango huo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Prof. Najat Mohammed wakati akifungua kikao cha Kwanza cha Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa kuzalisha umeme kwa kutumia Nishati ya Nyuklia (NEPIO) kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma.

Akifungua kikao hicho Prof. Najat Mohammed ameitaka kamati hiyo kuhakikisha wanaanza maandalizi mapema ili kukamilisha mpango huu ndani ya miaka saba.

“Matayarisho ya mpango huu yanachukua miaka 10 lakini sisi tunataka tuende miaka saba ili kupata umeme huu kwa muda mfupi zaidi hivyo niwatake muanze maandalizi mapema ili mfanye utafiti wa rasilimali zitakazotumika ili kama rasilimali hizo zinapatikana hapa nchini zitumike rasilimali zetu,” amesisitiza Prof. Najat.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *