Nchini Israel, utata unaongezeka kuhusu uchunguzi wa mauaji ya Oktoba 7. Je, mtu anaweza kuwa jaji na mtuhumiwa? Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ataongoza tume itakayofafanua mamlaka ya uchunguzi huu, ingawa yeye mwenyewe anaweza kuhusika kwa uchunguzi huo. Uamuzi huu umeonekana kama uchochezi na upinzani na familia za waathiriwa, ambao wanaulaani kama jaribio la “kufutiwa makosa” kisiasa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tovuti ya habari ya Ynet, Waziri Mkuu wa Israel ameteuliwa kuongoza chombo hiki, ambacho kitaanza kukutana Jumatatu, Desemba 22. Lengo la muungano tawala liko wazi: kuchukua nafasi ya tume huru ya uchunguzi, iliyoamriwa na sheria, na tume ya kisiasa ambayo wanachama wake wangeidhinishwa na serikali.

Kutokana na habari hii, upinzani umeungana na kutangaza kususia kabisa shughuli za seikali. Yair Lapid, kiongozi wa upinzani, analaani “tume ya kuficha ukweli,” anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalemu, Michel Paul.

Maneno hayo ni makali zaidi kutoka kwa Mkuu wa zamani wa jeshi Yair Golan, kiongozi wa chama cha Democratic, anayezungumzia “uhalifu uliopangwa chini ya kivuli cha sheria,” huku Naftali Bennett, kiongozi mwingine mkuu wa upinzani, akifupisha upuuzi wa hali hiyo: “Wale wanaopaswa kuchunguzwa huteua wachunguzi wao wenyewe.”

Hasira pia inaongezeka miongoni mwa wale walioathiriwa moja kwa moja: zaidi ya mateka 200 wa zamani na jamaa za waathiriwa wamesaini barua kali. Wanadai kukomeshwa mara moja kwa kile wanachokiita kujisafisha kisiasa na wanatoa wito wa kuanzishwa mara moja kwa tume huru ya serikali.

Kulingana na kura za maoni, zaidi ya 70% ya Waisraeli wanaunga mkono kuundwa kwa tume ya kitaifa ya uchunguzi ili kubaini jukumu la kushindwa kulikoruhusu Hamas kuvunja kizuizi kinachodaiwa kuwa kisichoweza kupenyeka kuzunguka Ukanda wa Gaza. Hii iliwezesha kundi la Palestina kuanzisha mauaji kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7, 2023.

Tume za kitaifa za uchunguzi si jambo la kawaida nchini Israel. Ile iliyoanzishwa baada ya Vita vya Waarabu na Israel vya mwezi Oktoba 1973, ambapo nchi hiyo ilikamatwa bila kutarajia na shambulio la pamoja kutoka Misri na Syria, ilisababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Golda Meir mnamo 1974. Kwa mujibu wa sheria, uamuzi wa kuunda tume ya uchunguzi ya serikali unategemea serikali, lakini wanachama wake lazima wateuliwe na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu. Taasisi hii inashutumiwa na Benjamin Netanyahu na washirika wake kwa kuwa na uadui naye kiasili.

Mnamo Novemba 10, Waziri Mkuu wa Israel alikataa tena wazo hilo, mbele ya wabunge, la kuunda tume ya uchunguzi ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *