Jeshi la Polisi nchini, kupitia kikosi cha Usalama Barabarani limeanza kufanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni hatua ya kudhibiti na kuzuia ajali za barabarani kufuatia ongezeko kubwa la idadi ya wasafiri kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumza leo na madereva katika Stendi Kuu ya Mabasi mkoani Arusha, Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Joseph Mwakabonga, amesema kuwa kipindi cha mwisho wa mwaka huambatana na kuongezeka kwa ajali za barabarani, hali inayochangiwa na baadhi ya madereva kuwa na mihemko ya kusafirisha abiria wengi kwa muda mfupi, jambo linaloongeza hatari ya ajali.
ACP Mwakabonga amebainisha kuwa operesheni hiyo inaendelea nchi nzima, ikilenga kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria, pamoja na kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates