Kulingana na ripoti, Wiz Khalifa alishtakiwa nchini Romania mwaka 2024 baada ya kuvuta bangi jukwaani wakati wa tamasha la Beach, Please!.
Ripoti za hivi karibuni zinaeleza kuwa mahakama ya Romania imetoa hukumu ya kifungo cha miezi tisa jela, ingawa uamuzi huo ulitolewa akiwa hayupo (in absentia). Timu yake ya wanasheria imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Kwa Sheria za Romania Bangi haijaruhusiwa kuvutwa hadharani kama alivyofanya Wiz Khalifa mwaka 2024.
Ikumbukwe kwamba huyu NI mwanamuziki wa Hiphop kutoka Marekani na mtindo wa uvutaji marijuana kwake yeye ni Sawa Maana marekani baadhi ya majimbo walihalalisha Bangi kama New Jersey, Arizona n.k
Wiz Khalifa Kwa sasa, hayuko kizuizini kulingana na ripoti mbalimbali za kimataifa Juu ya habari mbaya Kwa Wizy.
Tuachie maoni yako hapa chini.
@showtimerfa