Kocha maarufu wa timu ya ligi kuu ya Uingereza ya Mancester City kwa mara nyingine tena ameonesha uungwana na amechukua hatua ya kibinadamu ya kuwahami na kuwakingia kifua wananchi madhlumu wa Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Pep Guardiola anahesabiwa kuwa muungaji mkono maarufu zaidi wa Palestina kwenye fani ya mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa ripoti ya leo Ijumaa ya mwandishi wa gazeti la kila siku la Marca la Uhispania, Leila Hamed, kocha huyo ametangaza kuwa atahudhuria tamasha la kuiunga mkono Palestina huko Barcelona.

Kocha wa Manchester City ameshatangaza kuwaunga mkono watu wa Palestina na Ghaza mara saba kwa njia tofauti katika miezi sita iliyopita.

Mwezi uliopita, wakati timu ya taifa ya Palestina ilipokwenda Uhispania kucheza mechi mbili za hisani dhidi ya timu za Catalonia na Basque, Guardiola aliwahimiza watu wa nchi yake kuhudhuria kwa wingi kenye mechi hizo, na mwito wake ulipelekea kukusanywa zaidi ya dola milioni 2 za kuwasaidia wananchi wa Ghaza.

Mwandishi wa habari za Michezo, Leila Hamed, ameripoti pia kwamba, tamasha hilo limeandaliwa na kundi la “Act x Palestine” ili kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati za Wapalestina na litafanyika Barcelona Januari 29, 2026.

Kwa mujibu wa mwandishi huyo wa habari za michezo za gazeti la Marca la Uhispania, Pep Guardiola ndiye mtu mashuhuri zaidi na wa kwanza kujitolea kuhudhuria tamasha hilo ili watu wengi zaidi waweze kushiriki na kuweze kuchangishwa fedha nyingi zaidi kwa ajili ya wananchi madlumu wa Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *