BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu (WRBWB) imeeleza kuwa hali ya wingi wa maji katika Mto Ruvu inaendelea kuimarika kufuatia ongezeko kubwa la maji linalotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya bonde la mto huo.

Mwenyekiti wa WRBWB, Nickson Lutenda, amesema hayo alipokuwa akikagua vyanzo vyote vinavyotiririsha maji  katika Mto Ruvu, ili kutathmini mwenendo na hali halisi ya upatikanaji wa maji.

Lutenda amebainisha kuwa kwa sasa kiwango cha maji katika Mto Ruvu kimeongezeka kwa kiasi kikubwa, hali inayoonesha dalili njema za kurejea kwa hali ya kawaida ya upatikanaji wa maji, na kuwatoa hofu wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa maji.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwa watulivu na wenye subira katika kipindi hiki cha mpito, akisisitiza kuwa wataalamu wanaendelea kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inarejea na kuimarika kama ilivyokuwa awali.ruvruvu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *