Dar es Salaam. Msimu wa mwisho wa mwaka ndio huu umefika. Kawaida hiki ni kipindi cha furaha, tafakari na kukutana na familia. Kwa mastaa, licha ya maisha yao ya umaarufu na ratiba zenye pilikapilika, kipindi hiki huibua simulizi nyingi za kufurahisha ambazo huwafanya waonekane wa kawaida kama watu wengine.

Miongoni mwa mastaa wanaotajwa sana kipindi hiki cha Krismasi ni Mariah Carey. Kila ifikapo Desemba, wimbo wake All I Want for Christmas Is You huibuka upya kwenye chati za muziki duniani.

Mashabiki hufanya mzaha kuwa Mariah “huamka usingizini” mara moja kwa mwaka, huku yeye mwenyewe akifurahia utani huo na kuutumia kuwasalimu mashabiki wake mitandaoni.

Kwa upande wake, Rihanna hupendelea kusherehekea Krismasi na familia kuliko kufanya  sherehe ya kifahari.

Staa huyo wa kimataifa hurejea Barbados kukaa na familia yake, kupika vyakula vya asili na kufurahia muziki nyumbani. Simulizi hizi huwavutia mashabiki  na kufanya wamuone kama mtu wa kawaida.

Dwayne’The Rock’ Johnson naye amejijengea sifa ya kuwa na moyo wa kutoa msimu huu. Katika moja ya Krismasi, alimshangaza shabiki yake kwa kumpatia zawadi ya gari jipya, kitendo kilichosambaa mitandaoni na kuwasisimua wengi.

Tukio hilo lilionyesha kuwa Krismasi kwa mastaa wengine ni muda wa kugusa maisha ya wengine.

Kwa upande wa wachekeshaji, Kevin Hart amewahi kusimulia mikasa yake ya kuchekesha ya Krismasi, ikiwemo kujikuta kwenye hali ya aibu baada ya sherehe za kifamilia.

Kama lile tukio la jinsi alivyowahi kujifungia chooni kwa bahati mbaya siku ya Krismasi alipokuwa amelewa kidogo kwenye sherehe ya familia. Tukio hilo limekuwa sehemu ya  huwafanya mashabiki wake wacheka kila anapolielezea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *