
Hii ni licha ya kukosekana kwa uungwaji mkono wa kutosha katika mkutano wa kilele wa Umoja huo.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen alitarajiwa kusafiri kwenda Brazil kwa hafla ya kutia saini makubaliano kesho Jumamosi, lakini hilo lilitegemea idhini ya idadi kubwa ya nchi wanachama wa EU.
Ombi la Italia la kutaka muda zaidi lilisababisha kukosekana kwa uungwaji mkono wa kutosha kuhusu makubaliano hayo ya kibiashara.
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amesema katika taarifa kuwa, nchi yake iko tayari kuyaunga mkono makubaliano hayo endapo masuala yanayohusu sekta ya kilimo yatapatiwa ufumbuzi.