Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kristi Noem ameandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba mshukiwa huyo, Manuel Neves Valente, aliingia Marekani kupitia mpango wa bahati nasibu ya viza ya uhamiaji mnamo mwaka 2017 na baadae kupewa kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini humo.

Amesema ameusimamisha mpango huo ili kuhakikisha hakuna Wamarekani zaidi watakaodhurika.

Claudio Neves Valente, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 48, anaripotiwa kuvamia jengo la chuo kikuu cha Brown mnamo Desemba 13 na kufyatua risasi kwa wanafunzi waliokuwa wakifanya mitihani, na kusababisha vifo vya watu wawili na kuwajeruhi wengine tisa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, mpango wa bahati nasibu ya uhamiaji hutoa hadi viza 55,000 kila mwaka kwa watu “kutoka nchi zenye viwango vya chini vya uhamiaji kwenda kuishi na kufanya kazi Marekani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *