Serikali kupitia Wizara ya Fedha imepiga marufuku wataalamu wasiokuwa na sifa na taaluma ya ununuzi na ugavi kupewa nafasi za kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za umma, hususan katika ngazi ya halmashauri.

Hatua hiyo inalenga kudhibiti upotevu wa fedha za umma unaosababishwa na ukosefu wa weledi katika utekelezaji wa majukumu ya ununuzi na ugavi.

Changamoto hiyo ilibainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Bodi unaofanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku tatu.

Alieleza kuwa uwepo wa baadhi ya watumishi wasio na sifa za kitaaluma katika idara za ununuzi na ugavi, hususan katika ngazi ya halmashauri, umekuwa ukikwamisha utendaji kazi wenye ufanisi na kuchangia hasara pamoja na upotevu wa fedha za umma.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *