Watu zaidi ya 50,000 wamekuwa wakimbizi wapya tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba huku mapigano yakikithiri, Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) lilionya siku ya Ijumaa, likisema raia raia wanakimbia kwa hofu siyo kwa kupenda kwao.

“Watu nchini hawaondoki kwa kupenda, wanakimbia kwa ajili ya usalama,” alisema Mohamed Refaat, mkuu wa Shirika la IOM nchini Sudan, akizungumza na waandishi wa habari walioko Geneva kutoka Port Sudan.

Refaat alisema wanaoondoka katika makazi yao Kordofan ni kutokana na kuongezeka kwa vita, huku wakazi wakikimbia kutoka miji ikiwemo Babanousa, Kadugli na El-Obeid.

Alizungumzia ripoti za wapiganaji wa RSF pamoja na washirika wao wa Sudan People’s Liberation Movement-North kushambulia majengo ya makazi ya watu katika maeneo ya Dilling, Kordofan Kusini, katika kipindi cha saa 48 iliopita.

Wanawake na watoto

RSF imekuwa ikipigana na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023, kufuatia kusamvaratika kwa utawala wa mpito wa kiraia. Oktoba 26, vikosi vya RSF vilivamia Al Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, baada ya kuwafungia watu kwa siku 500, kusababisha watu wengi kuondoka katika makazi yao na wengine kukwama wakiwa hawana chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *