Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 2
Manchester United itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaj i wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo mwezi Januari na wanatumai kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City kunaweza kuongeza nafasi yao ya kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph – usajili unahitajika)
Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Ruben Neves, 28, amesusia kutia saini mkataba mpya na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Pro League. Tetesi zinaseama anataka kurejea Ulaya huku Manchester United ikionekana kuwa shabaha ya kiungo huyo wa zamani wa Wolves. (Times – usajili unahitajika)
Manchester United iko tayari kumuuza Kobbie Mainoo, 20, katika dirisha la uhamisho wa Januari ikitapata ofa nzuri. Unite inasita kumruhusu kiungo huyo wa kati wa Uingereza kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports)
Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca, 45, anaongoza wagombea ambao Manchester City inawafikiria iwapo kocha Pep Guardiola, 54, ataondoka Etihad msimu ujao. (Athletic – michango inahitajika)
Saint-Etienne wamekataa ofa ya awali ya euro milioni nane (£7m) kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Djylian N’Guessan, 17, lakini klabu hiyo inafikiria kumuuza mshambuliaji huyo wa Ufaransa kwa euro 12.5m (£11m). (L’Equipe – kwa Kifaransa),
Mchezahi mahiri Mholanzi AZ Alkmaar Kees Smit, 19, ni mmoja wa viungo wanne wanaofuatiliwa na Newcastle, huku mlinzi wa Toulouse Mfaransa Dayann Methalie, 19, pia anadhaniwa kuwa kwenye orodha yao. (Mail – usajili unahitajika)