ARUSHA; MKURUGENZI Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Soter Salema amesema kampuni hiyo inajivunia safari ya mageuzi ya teknolojia ikiwemo utunzaji wa nyaraka, kumbukumbu za picha na historia mbalimbali.

Salema amesema hayo leo jijini Arusha mara baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Munde kutembelea banda la maonesho la TSN na kujionea shughuli mbalimbali za magazeti katika Mkutano wa 16 wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) unaofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) .

Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Munde akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Soter Salema kuhusu shughuli mbalimbali za kampuni hiyo, alipotembelea banda la TSN kwenye Mkutano wa 16 wa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) leo Desemba 19, 2025.

Amesema TSN inajivunia kuhifadhi nyaraka ikiwemo kuzipanga na kuhifadhi kwa usalama na kuhakikisha taarifa zinapatikana kwa matumizi ya baadaye, ikiwemo kulinda kumbukumbu za kihistoria, kisheria au kitaasisi.

“TSN tunahakikisha tunatumia Tehama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) katika kuhakikisha nyaraka za serikali zinahifadhiwa kwa usalama sanjari na utunzaji wa vitabu vyenye historia mbalimbali,” amesema.TSN pia imepokea tuzo maalum ya shukrani kutokana na kudhamini mkutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *