
Polisi wa Ufaransa wamevamia nyumba ya Waziri wa Utamaduni, Rachida Dati, pamoja na makao makuu ya wizara na ofisi yake katika manispaa ya Paris, kufuatia kufunguliwa uchunguzi dhidi yake kuhusu tuhuma za ufisadi, utumiaji mbaya wa madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma.
Dati, mwenye umri wa miaka 60, anatuhumiwa kupokea takriban euro 300,000 ($343,000) katika malipo yasiyotangazwa kutoka kwa kampuni kubwa ya nishati GDF Suez wakati wa kipindi chake kama mbunge wa Bunge la Ulaya kati ya 2010 na 2011. Dati amekanusha mashtaka yote dhidi yake.
Uvamizi huo ulikuja baada ya uchunguzi kufunguliwa Oktoba 14 dhidi ya Dati, kwa tuhuma za ufisadi, utumiaji mbaya wa madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma.
Rachida Dati na wakili wake hawakuweza kupatikana kutoa maoni juu ya suala hili. Dati anatazamiwa kuwa mgombea mkuu wa umeya wa Paris katika uchaguzi wa mwaka ujao, 2026.