Viongozi wa EU hata hivyo bado hawajafikia mwafaka na Ubelgiji kuhusu pendekezo la kutumia mali za Urusi zilizozuiwa ndani ya Umoja huo kama chanzo cha kukusanya fedha za mkopo huo.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu mbele, akibainisha kuwa kukopa kupitia masoko ya mitaji ndio chanzo halisi na kinachowezekana zaidi kwa wakati huu ili kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, pia amepongeza uamuzi huo wa viongozi wa Umoja wa Ulaya wa kuipatia Ukraine mkopo usio na riba.

“Ulaya imeupokea ujumbe. Ulaya imeonyesha uwezo na mamlaka yake. Tunasimama imara dhidi ya tishio kubwa zaidi kwa usalama barani Ulaya — uchokozi wa Urusi ambao kwa muda mrefu umevuka mipaka zaidi ya uvamizi dhidi ya Ukraine,” amesema Merz.

Baada ya takriban miaka minne ya vita, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linakadiria kuwa Ukraine itahitaji euro bilioni 137 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *