Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR imeeleza katika ripoti yake kwamba “ilirekodi mauaji ya raia 1,013 wakati wa mashambulizi ya RSF kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam kati ya Aprili 11 na 13.”

Ripoti hiyo imeongeza kuwa zaidi ya wakimbizi 400,000 waliokuweko kwenye kambi hiyo walilazimika kukimbia wakati wa mashambulizi hayo ya siku tatu.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF yamesababisha takriban watu milioni 12 kuyahama makaazi yao nchini Sudan huku maelfu ya wengine wakikabiliwa na kitisho cha njaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *